Rais Samia afarijika kuona 58% ya wahitimu ni wanawake

HomeKitaifa

Rais Samia afarijika kuona 58% ya wahitimu ni wanawake

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuleta mabadiliko chanya katika jamii mara wanapohitimu masomo yao.

Ameyasema hayo leo mjini Zanzibar katika Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na kueleza kuwa amefarijika kuona wanawake wanazidi kuhamasika katika elimu.

“Nimepata faraja kuona asilimia 58 ya wahitimu leo ni wanawake,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD) ya Usimamizi wa Utalii na Masoko ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuinua utalii kabla ya kuwa Rais na hata wakati wa urais kupitia Royal Tour.

“Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa nimesimama mbele ya umma huu kukubali Shahada hii.” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!