Rais Samia achangia Sh. milioni 150 ujenzi wa kanisa Machame

HomeKitaifa

Rais Samia achangia Sh. milioni 150 ujenzi wa kanisa Machame

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 150 kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT la Bethel Usharika wa Nshara Machame Mkoani Kilimanjaro anakosali Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Akizungumza leo katika ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo, Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye husali katika Kanisa hilo awapo nyumbani Machame amesema alishirikisha Watu mbalimbali kuhusu kuchangia ambapo miongoni mwao ni Rais Samia.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge na Wananchi mbalimbali leo wamejitokeza katika ibada ya harambee kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT Machame Nshara, harambee ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye pia ni Msharika wa Kanisa hilo.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Adolph Mkenda, Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe na Wabunge wa Viti maalum Easter Bulaya na Halima Mdee.

error: Content is protected !!