Rais Samia Suluhu Hassan, akiendelea na ziara yake wilayani Muheza, mkoa wa Tanga, alifanya kitendo kilichogusa hisia za watu wengi baada ya kumpisha mtoto akalie kiti chake cha Urais kwa muda.
Tukio hilo lililovuta hisia za wananchi lilionyesha upendo na unyenyekevu wa Rais Samia kwa watoto, huku likitafsiriwa kama ishara ya matumaini kwa kizazi kijacho cha taifa. Katika video na picha zilizosambaa mitandaoni, Rais Samia alionekana akitabasamu wakati mtoto huyo akiketi kwenye kiti chake kwa furaha.
Wananchi wengi wamepongeza kitendo hicho, wakikitafsiri kama ujumbe wa kuwaandaa watoto kuwa viongozi wa baadaye. Wengine walisisitiza kuwa hatua hiyo inaonyesha uongozi wa karibu na wananchi, unaohamasisha upendo na mshikamano katika jamii.