Waziri wa Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia vijiji 75 vilivyokuwa katika migogoro ya matumizi ya ardhi katika Mkoa wa Arusha vibaki katika maeneo ha hifadhi.
“Vijiji na mitaa 116 Arusha kuachiwa vijiji 75 kubaki kwenye maeneo yake ni hisani ya kipekee na tunatakiwa tuiheshime na tusiitumie vinginevyo kwa sababu Mheshimiwa Rais Samia alikuwa na uwezo wa kutaka kuviondoa lakini ameridhia maeneo 75 kubaki,” alisema Dk Mabula.
Dk Mabula alisema uongozi wa mkoa utakuwa na jukumu la kusimamia mpango wa matumizi ya ardhi sambamba na kudhibiti vyanzo na vichocheo vya kuzalisha migogoro.
Alisema hayo alipozungumza na uongozi wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya mwaziri wa wizara za kisekta mkoani humo.