Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 1,2022 amewaapisha viongozi wateule Ikulu, Dar es Salaama na kutaja vigezo anavyotumia kuteua viongozi hao.
“Ninapofanya teuzi hizi, siangalii kabila la mtu, rangi ya mtu wala anakotoka, naangalia sifa, uwezo, uaminifu wake kwa nchi na serikali hii, sasa katika teuzi hizi kama kuna mtu hakuridhika yanayoniongoza ni hayo, siangalii makundi sababu hata mimi sina kundi,”
“Kama kuna mtu hakuridhika kwa njia moja au nyingine ile, yanayoniongoza ni hayo, siangalii makundi sababu mimi sina kundi, na ninadhani mkijitizama mlioteuliwa kama mna makundi yenu humo utajikuta kabisa mko mchanganyiko.” amesema Rais Samia Suluhu.
Aidha, Rais Samia amewasihi viongozi hao wakafanyaje kazi kwa bidii na kujali maslahi ya wananchi huku akiahidi kuwafatilia kwa ukaribu utendaji kazi wao katika maeneo yao ya kazi.
“Mimi ninalofanya ni kuteua Watanzania ambao nahisi hawa tutasaidiana katika kufanya kazi kuhudumia wananchi kuleta maendeleo katika Taifa hili, sina vigezo vingine, mengine hayo kwa mamlaka niliyopewa na Katiba siangalii.” amesema Rais Samia Suluhu.