Rais Samia ataka mifumo ya ulipaji kodi iwe ya haki

HomeBiashara

Rais Samia ataka mifumo ya ulipaji kodi iwe ya haki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amezindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi leo Oktoba 4, 2024 Ikulu Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Samia amesema lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kusaidia kufanyika kwa tathmini mfumo mzima wa kodi ili uweze kuimarishwa.

Rais Samia amesema, azma ya serikali ni kuwa na mfumo unaotoa haki ambapo kila mtu anayepaswa kulipa kodi atalipa kodi stahiki.

“Jambo kubwa na la msingi kwetu ni kwamba tunataka kujenga mfumo wa haki unaotenda haki ambapo kila anayestahili kulipa kodi, alipe kodi stahiki,” amesma Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewasihi watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanalipa kodi huku akisisitiza kwamba kodi ni damu ya serikali.

 

error: Content is protected !!