Rais Samia atangaza ujio wa Filamu ya The Hidden Tanzania

HomeKimataifa

Rais Samia atangaza ujio wa Filamu ya The Hidden Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kwamba vivutio ambavyo havikuonyeshwa kwenye awamu ya kwanza ya filamu ya Royal Tour iliyokuwa ikionyesha utalii wa Tanzania, vitawekwa kwenye awamu ya pili inayoitwa The Hidden Tanzania.

Mkuu huyo wa nchi amesema waandaaji tayari wanampango wa kuja na awamu ya pili ambayo itaonyesha maeneo ya Tanzania yaliyojificha.

” Waandaaji wameshakuja na mpango wa awamu ya pili na wameipa jina The Hidden Tanzania yani maeneo mengine ya Tanzania yaliyojificha, ni kwenda kuyachukua na kuyaonyesha kwamba Tanzania mbali ya tuliowaonyesha lakini bado kuna mambo haya.” amesema Rais Samia.

Amezungumza wakati akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara.

 

error: Content is protected !!