Novemba 24,2022 akifungua Mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Wansheria Afrika Mashariki jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliahidi kukipatia Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) eneo la kujenga ofisi zao baada ya kuwasilisha ombi.
Leo Agosti 14,2023 Rais Samia ametimiza ahadi yake kwa kumkabidhi Harold Sungusia, Rais wa TLS hati ya kiwanja kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zao mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino.
Tangu kuingiwa kwake madarakani, Rais Samia amekua akitimiza yale mambo mengi aliyoyaahidi uku akiendelea kufanyia kazi mengine. Mfano aliahidi kuhakikisha uchumi unakua, aliahidi kumtua mama ndoo, aliahidi kutoa fedha kwa timu za Simba na Yanga kwenye mashindano yao ya kimataifa ahadi alisema inaenda kwa timu nyingine pia.