Rais Samia Suluhu Hassan alifika Jakarta leo kuanza ziara ya kiserikali nchini Indonesia. Nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia imeendelea kuwa na uhusiano imara na Tanzania, hasa katika sekta ya nishati, kilimo, na uchumi wa bluu.
Mwaka uliopita, nchi zote mbili zilisaini Mikataba Saba ya Makubaliano (MoUs) inayolenga kukuza sekta za nishati, uvuvi, mifugo, kilimo, ulinzi, afya, na utalii.
Nchi zote zimekubaliana kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu ili kurahisisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Rais Samia anatarajiwa kuondoka Indonesia tarehe 26 Januari 2024.