Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Hoteli ya Kitalii ya Bawe Island the Cocoon Collection iliyopo katika Kisiwa cha Bawe, Zanzibar yenye hadhi ya nyota tano.
Hoteli hiyo imezalisha ajira 400 ambapo wanufaika wakubwa wa ni wazawa ambao wengi wao ni wavuvi waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika kisiwa hicho.
Pia Rais Samia, amesifu uongozi wa mradi huo kwa uamuzi wa kuwekeza Bawe.
Sifa kubwa ya mradi huo ni namna unavyotunza mazingira kwani unatumia nishati ya umeme wa jua (solar power) na pia maji ya bahari wanayotumia baada ya kuyatibu.
Aidha, Rais Samia amewaagiza wahusika wa mradi huo kuendelea kutunza mazingira.