Rais Samia: Haki izingatiwe Uchaguzi Mkuu 2025

HomeKitaifa

Rais Samia: Haki izingatiwe Uchaguzi Mkuu 2025

Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka umma wa Watanzania na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha haki inasimamiwa kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Akihutubia Kongamano la Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema maslahi ya taifa lazima yawekwe mbele kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja.

“Neno haki ni lakulitilia sana maanani. Kwa niaba ya Watanzania wote, ujumbe wetu kwa Tume ya Uchaguzi ni kusimamia haki na kutenda haki,” alisema.

Rais aliongeza kuwa Tanzania inapaswa kuendelea kubaki imara hata baada ya uchaguzi.
“Nchi yetu kwanza na sisi binafsi zetu ni baadaye. Tuitangulize Tanzania na kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi,” alisema.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa amani akieleza kuwa amani siyo kukosekana kwa migogoro, bali ni njia ya kuiondoa kwa utulivu.

Kongamano hilo limewakutanisha viongozi wa kisiasa, dini, asasi za kiraia na vijana, likiwa na kaulimbiu ya kudumisha mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

error: Content is protected !!