Wizkid hali mbaya

HomeBurudani

Wizkid hali mbaya

Msanii kutoka nchini Nigeria, Wizkid amekosa tuzo katika vipengele viwili vya Best Global Music Performance na Best Global Music Album jambo lililoibua hisia pinzani kutoka kwa mashabiki wake kwani walitegemea atanyakua tuzo hizo.

Tuzo ya Best Global Music Performance imenyakuliwa na Angelique Kidjo ambaye mara kwa mara amekuwa akiibuka mshindi wa tuzo hizo za Grammy na kuwapiku manguli wengi.

Mmoja wa watu waliopaza sauti kuhusu tuzo hizo ni mwanasheria wa Davido, Bobo F. Ajudua ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter aliandika kwamba kila mtu anajua kwamba tuzo hiyo angepaswa kupewa Wizkid kutokana na wimbo wake wa ‘Essence’ uliofanya vizuri dunia nzima kwa muda mrefu na kushika chati namba moja kwenye mitandao tofauti.

Ikumbukwe Tuzo za Grammy za mwaka 2020, Burna Boy pia alipigwa chini na mwanamama huyu Angelique Kidjo kwenye kipengele cha Wimbo bora Kimataifa.

Newer Post
Older Post
error: Content is protected !!