Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa

HomeKitaifa

Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa

Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kugharamia matibabu ya Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ambaye alitekwa na kurejuhiwa vibaya na watu waisojulikana.

Zitto amesema ameongea na Rais Samia na kumshauri kufanyia uchunguzi suala hilo jambo ambalo Rais Samia amekubali kufanyia kazi.

“Nimemnasihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama juu ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii. Kama Taifa, tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili” Ameeleza Zitto katika taarifa hiyo.

Kulingana na Zitto Kabwe, Rais Samia ameahidi kufanyia kazi ushauri wake na kwamba Rais binafsi ameeleza kuwa atabeba gharama zote za matibabu ya Sativa kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa jambo hilo.

 

error: Content is protected !!