Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru leo kinamtuku Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, shahada ya heshima. Rais yupo kwenye ziara ya siku nne nchini India.
Taarifa kutoka Wizara ya Elimu ya India imesema Chuo “Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania ataheshimiwa na shahada ya heshima (Honoris Causa) kutoka Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwa jukumu lake muhimu katika kukuza uhusiano imara kati ya India na Tanzania, kukuza diplomasia ya kiuchumi, na kufanikiwa katika kuimarisha ujumuishaji wa kikanda na kimataifa. Anajivunia kuwa ‘matokeo ya elimu ya Kihindi’, akiihusisha na mafunzo yake ya ITEC huko NIRD, Hyderabad,” Wizara ya Elimu ilichapisha kwenye mtandao wa kijamii X (uliokuwa ukitambulika kama Twitter).
H.E. Dr. @SuluhuSamia, the first woman President of Tanzania, will be honored with an Honorary Doctorate (Honoris Causa) by Jawaharlal Nehru University for her pivotal role in fostering stronger India-Tanzania relations, promoting economic diplomacy, and achieving success in… pic.twitter.com/acLSd3Tr7C
— Ministry of Education (@EduMinOfIndia) October 9, 2023
Waziri Mkuu Narendra Modi alifanya mazungumzo ya kina na Rais Samia wa Jumatatu, akilenga kuimarisha uhusiano wa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Kabla ya mazungumzo hayo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Arindam Bagchi, alisema ziara ya rais wa Tanzania ni fursa ya kuchukua uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili “kwenye viwango vipya”.