Lengo ni kufikia uwekezaji wa Dola bilioni 3 ifikapo 2025

HomeKimataifa

Lengo ni kufikia uwekezaji wa Dola bilioni 3 ifikapo 2025

Tanzania inalenga kuongeza uwekezaji kutoka India ambaye ni mshiriki wake mkubwa katika biashara.

Inatarajia uwekezaji kutoka India kupanda hadi dola bilioni 3 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025 kutoka dola milioni 300 za sasa.

Hayo yamebainishwa na Rais Samia Suluhu alipokuwa akizungumza katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India Jijini New Delhi

Aidha, Rais Dkt. Samia pamoja na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wamekubaliana kupunguza urasimu na kuimarisha zaidi uhusiano.

error: Content is protected !!