Rais Samia kwenda Marekani kushiriki Mjadala wa Norman E.Borlaug

HomeKimataifa

Rais Samia kwenda Marekani kushiriki Mjadala wa Norman E.Borlaug

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hii leo tarehe 29 Oktoba 2024, anatarajia kuondoka nchini kuelekea Des Moines, nchini Marekani kuhudhulia mjadala wa kimataifa wa Normal E. Borlaug ulioandaliwa na Taasisi ya Wood Food Prize Foundation ya nchini humo.

Taarifa kutoka Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia atakuwa ni miongoni mwa Marais wanne kutoka Afrika, waliopewa heshima ya kushiriki na kuchangia kwenye mjadala huo.

Mbali na mjadala huo, Rais Samia pia atashiriki hafla ya utoaji tuzo ya World Food Prize kwa mwaka 2024, kwa watu wenye mchango mkubwa kwenye sekta ya Kilimo.

error: Content is protected !!