Rais Samia: Maamuzi ya wapiga kura yaheshimiwe

HomeKitaifa

Rais Samia: Maamuzi ya wapiga kura yaheshimiwe

Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza kuheshimiwa kwa maamuzi ya wapiga kura akieleza kwamba demokrasia yenye nguvu hujengwa kwa misingi ya heshima na mshikamano.

Amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu zoezi la Uchaguzi wa Serikalii za Mitaa litakalofanyika kesho Novemba 27,2024.

Rais Samia ameeleza nia ya serikali yake kwamba ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopo.

Pia, amewasihi wananchi kujiepusha na vitendo vya uchochezi, vurugu au uvunjifu wa sheria siku ya kesho ili zoezi hilo liweze kufanyika vizuri.

error: Content is protected !!