Rais Samia: Nendeni mkajiongeze na kuviishi viapo vyenu

HomeKitaifa

Rais Samia: Nendeni mkajiongeze na kuviishi viapo vyenu

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi aliowateua hivi karibuni kwenda kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi na kuishi kwa kufuata viapo walivyokula. Akizungumza katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa viongozi hao kujiongeza kwa kutumia utaalamu walioupata pamoja na kutumia busara zao katika utendaji wa kazi.

“Mabadiliko haya ni ya kawaida, ni kuongeza ufanisi katika maeneo yetu na Makamu wa Rais amesema vizuri tunachotarajia kwenu ni ufanisi kwenda kuongeza ufanisi kwenye maeneo yenu,” alisema Rais Samia.

Aidha, aliwakumbusha viongozi hao juu ya viapo walivyokula na kuwasihi kuhakikisha wanavifuata kwa uadilifu pamoja na maadili ya kikazi yanayotakiwa. Rais Samia pia aliwahimiza kutumia akili ya kawaida (common sense) katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.

“Mmeapa viapo viwili hapa… muende mkaishi na viapo hivyo lakini pia mkafuate maadili ya kikazi yanayotakiwa,” aliongeza Rais Samia.

error: Content is protected !!