Rais Samia: Tamasha la Kizimkazi ni chachu ya maendeleo kwa wananchi

HomeKitaifa

Rais Samia: Tamasha la Kizimkazi ni chachu ya maendeleo kwa wananchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Tamasha la Kizimkazi limeendelea kujipambanua kuwa tamasha la kimaendeleo kutokana na mchango wake katika utekelezaji wa miradi yenye manufaa kwa wananchi.

Akizungumza katika ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi, Rais Samia alieleza matumaini yake kuhusu mchango wa tamasha hilo kwa mwaka huu. “Tunamatumaini kwamba Tamasha la Kizimkazi la mwaka huu pia limechochea maendeleo kwa sababu kuna miradi mingi ambayo itakwenda na inaendelea kuzinduliwa,” alisema Rais Samia.

Aidha, aliwahakikishia wakazi wa Wilaya ya Kusini kwamba tamasha hilo litakuwa na athari chanya kwa maeneo yote ya wilaya hiyo. “Nataka niwahakikishe ndugu zangu wa Wilaya ya Kusini kwamba tamasha hili litagusa kila pahali ndani ya Wilaya ya Kusini, kila pahali jinsi tutakavyoweza ndani ya Wilaya ya Kusini,” alisisitiza Rais Samia.

Tamasha la Kizimkazi limekuwa maarufu kwa kuchochea shughuli za maendeleo na kuvutia miradi mipya inayolenga kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

error: Content is protected !!