Rais Samia : Tunzeni siri za serikali

HomeKitaifa

Rais Samia : Tunzeni siri za serikali

Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watunza kumbukumbu na nyaraka nchini kuwa Serikali itawalinda kwa kutambua kada hiyo ni kitovu cha Serikali.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 27, 2022 jijini Arusha katika mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA).

Amewataka watunza kumbukumbu kutunza siri za Serikali kwa uadilifu na weledi, kwani wasipofanya hivyo watadhulumu haki za watu.

“Chukua picha wewe ni mtunza kumbukumbu kwenye sekta ya kilimo, kuna mambo ya ruzuku hufanyi uadilifu uaanacha kompyuta kaingia mtu mwingine kaingilia hizo taarifa, wakulima wanasubiri mbolea wewe taarifa ulizonazo si hizo zilizokusanywa kwenye field.

“Unawakosesha wakulima mbolea msimu unapita, tunakwenda bila chakula, akiba ya chakula hakuna angalia kosa lako dogo linavyoleta athari,” amesema.

Amesema kumekuwa na utaratibu mbovu wa nyaraka za Serikali kuwekwa mitandaoni, jambo alilosema linakwenda kinyume na utaratibu wa taalamu hiyo na kuleta athari katika utoaji haki za watu.

error: Content is protected !!