Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeitoza faini ya Sh milioni mbili luninga ya mtandaoni ya Zama Mpya kwa kosa la kuchapisha habari kuhusu tozo za serikali bila kuzingatia maadili, hivyo kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Pia imetoa onyo na kukiweka chini ya uangalizi wa TCRA kwa miezi mitatu, ili kuboresha utendaji kazi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Habi Gunze, alisema Agosti 12, mwaka huu, TCRA ilitoa leseni kwa Zama Mpya Tv na Agosti 28 mwaka huu walichapisha taarifa za uchochezi kuhusu tozo za serikali kwenye ukurasa wa twitter kinyume na kanuni ya 9 (a), 12 (a) (I) na 16 (1) aya 3 (a), (d), (g), (h) na (k) ya kanuni za kielektroniki na Posta ya mwaka 2020.