Rushwa nchini Kenya yadhoofisha uchumi

HomeKimataifa

Rushwa nchini Kenya yadhoofisha uchumi

Ripoti ya Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa ya Kenya (EACC) ya mwaka 2024 inaonesha kuwa rushwa bado ni tatizo kubwa linaloathiri moja kwa moja uchumi wa Kenya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi hupoteza hadi dola za Marekani bilioni 1.5 kila mwaka kutokana na rushwa, uzembe katika sekta ya umma na kunaswa kwa dola, hali inayopunguza uwezo wa serikali kugharamia maendeleo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa rushwa imeenea katika utumishi wa umma, ikijitokeza zaidi kupitia vitendo vya hongo, upendeleo, matumizi mabaya ya madaraka, ukabila, upendeleo wa kifamilia na ubadhirifu wa fedha za umma. Hali hiyo imesababisha kushuka kwa ukuaji wa uchumi, kuzorota kwa huduma za jamii na kuongezeka kwa gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imesema kuwa uporaji wa fedha za umma umelazimisha serikali kuongeza ukopaji ili kufidia mapengo ya bajeti, jambo lililopelekea kuongezeka kwa deni la taifa. Kwa sasa miradi mingi ya maendeleo nchini Kenya imekuwa ikipandishwa gharama kutokana na rushwa huku mikataba ya manunuzi ikitolewa kwa makampuni yasiyo na uwezo hali ambayo inayozidisha hasara kubwa kwa maendeleo ya uchumi nchini humo.

Ndani ya ripoti hiyo imetoa mapendekezo ya jumla ya kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha taasisi za uwajibikaji, kusimamia sheria na kujenga utamaduni wa uadilifu ili kudhibiti vitendo vya rushwa ambavyo kwa sasa vinadhoofisha uchumi wa Kenya na maisha ya wananchi na kurejesha imani ya umma na kukuza maendeleo endelevu .

error: Content is protected !!