Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa ratiba ya safari za treni ya kisasa ya SGR baada ya serikali kutan gaza kurejesha safari kutoka Dar es Salaam -Dodoma na Dodoma kwenda Dar es Sa laam kupitia Morogoro.
TRC ilitoa ratiba hiyo kwa safari za treni ya haraka na ya kawaida na safari hizo zilianza juzi saa 12:00 asubuhi kutoka stesheni ya Dar es Salaam, huku Dodoma safari zikianza saa 8:15 mchana na kuwasili Dar es Salaam saa 12:10 jioni jana.
Desemba 31, 2025 TRC ilisitisha kwa muda safari za treni ya SGR kati ya Morogoro na Dodoma kutokana na athari za mvua katika eneo la Kidete na Godegode.
Akuzungumza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba juzi, Waziri wa Uchu kuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema kwa sasa reli ipo salama baada ya serikali kufanya tathmini na kujiridhisha, imerudisha safari kama kawaida.
Alisema ni muhimu kuzingatia usalama wa wananchi kabla ya kuendelea na safari za treni ya SGR kutokana na mvua zilizonyesha.
“ Kwanza, reli yetu ipo salama lakini hatuwezi kuendelea kuumia bila kujiridhisha, kwa sababu jam bo la kwanza kwetu ni usalama wa wananchi,” alisema.
Alisema wataalamu wamefan ya marekebisho madogomadogo katika eneo la Kidete na na tayari tathmini imeshafanyika na hivyo kurejesha safari za treni hiyo.
Dk Mwigulu alisema usafiri wa treni ya kisasa inayotumia umeme unapaswa kuchukuliwa tahadhari, hasa wakati wa mvua zinaponye sha ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
“Tusifanye jambo la usafiri wa treni kwa mihemko. Duniani kote wanakotumia mindombinu hii ya kisasa, wananzingatia zaidi masuala ya usalama,” alisema.
Aliongeza: “Barabarani unaweza kukwama kwenye tope ukasukuma lakini kwenye treni kama mvua inayonyesha ni ya upepo, huwezi ruhusu treni kuendelea. Upepo unaweza kutikisa nyaya wakati treni inatembea.


