Katika Jimbo la Florida, Marekani, samaki aina ya ‘bonefish’ wamekutwa wakiwa wamelewa madawa mbalimbali ya binadamu.
Kati ya samaki 93 waliopimwa wote wamekutwa na walau aina moja ya madawa ya hospitali ikiwemo madawa ya moyo, fangasi na dawa za kuondoa sonono.
Samaki mmoja liyepimwa huko Key West alikutwa na aina 17 za madawa mara 300 zaidi ya viwango vya binadamu.
Aina nyingine ya samaki waliopimwa na kukutwa na madawa hayo ni uduvi.
Chanzo cha samaki hao kupata madawa kinaelekezwa kuwa ni mchafuko wa bahari kutokana na maji machafu kutoka viwanda vya dawa kuelekezwa baharini, maji ya mvua yanayobeba uchafu kupeleka baharini, lakini binadamu kuwa moja ya sababu kubwa utokana na vinyesi ambavyo maji yake huelekezwa kwenye vyanzo vya maji.