Moto wateketeza soko Temeke

HomeBiashara

Moto wateketeza soko Temeke

Soko la Vetereni lililopo Temeke, Dar es Salaam limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza vibanda vipatavyo 250 kati ya 453.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amethibitisha kutokea kwa moto huo na kusema serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Temeke akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo itachukua hatua za haraka ili wafanyabiashara hao warejee kwenye majukumu yao.

Chanzo cha moto katika soko hilo lililokuwa na  wafanyabiashara 803 kinasemekana kuwa ni hitilafu ya umeme.

error: Content is protected !!