Samia: wapeni raha wafanyabiashara

HomeUncategorized

Samia: wapeni raha wafanyabiashara

Rais Samia Suluhu amepiga marufuku wafanyabiashara kupewa ankara za kodi za miaka mitano hadi sita nyuma kwa kuwa hilo sio kosa lao bali ni la mamlaka zinazohusika na ukusanyaji.

Alitoa ahizo hilo wakati akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera na Watanzania kwa ujumla kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoani humo jana.

“Watoza kodi walikuwa wapi hadi wawatoze wafanyabiashara kodi za nyuma.”

“Achaneni na hiyo biashara ya kuwatoza watu kodi za miaka mingi nyuma, mnaweza tu kurudi hadi mwaka mmoja nyuma lakini si zaidi ya hapo, wapeni raha wafanyabiashara wafanye biashara zao vizuri, sisitizeni kodi za kuanzia sasa na kwenda mbele,” alisisitiza Rais Samia.

Aidha, alipiga marufuku wakulima kuuza kahawa nje ya nchi hasa nchi jirani kwa kuwa bei ya kahawa hapa nchini kwa sasa ni nzuri.

error: Content is protected !!