Watu 18 wafa ajali ya basi mafinga

HomeKitaifa

Watu 18 wafa ajali ya basi mafinga

Watu 18 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi dogo aina Costa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa , ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea vifo hivyo akisema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

“Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu 10 wamepoteza maisha papo hapo ,” amesema.

Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya watu walioko katika eneo la tukio wamesema mpaka saa tatu asubuhi ,jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.

SOURCE: MWANANCHI

 

error: Content is protected !!