Makamba: Si kweli, bei ya umeme haijapanda

HomeKitaifa

Makamba: Si kweli, bei ya umeme haijapanda

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kupanda kwa bei ya umeme si za kweli na Serikali inasikitishwa na wanaosambaza taarifa hizo.

Akijibu swali la Mbunge wa Nyasa Stella Manyanya, Waziri January Makamba amesema “si kweli kabisa kwamba bei ya umeme imepanda, Serikali inasikitishwa na wale wanaoeneza maneno hayo na uvumi huo kwenye mitandao na tumeomba Mamlaka husika zichukue hatua kwa udanganyifu na upotofu huo unaofanywa”

“Mchakato wa kupandisha bei ya umeme ni mrefu, unahusisha maombi ya TANESCO kwa EWURA na unahusisha public hearing kwamba Wananchi lazima wahusishwe na washirikishwe katika kutoa maoni yao pale bei ya umeme inapopandishwa, ni mchakato mrefu ambao hauwezi kufanyika kwa siri kwahiyo hizi taarifa kwamba Serikali imepandisha bei ya umeme sio kweli na naomba zipuuzwe” amesema Waziri Makamba

Mbali na Waziri Makamba, Shirika la Umeme limekanusha pia taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

error: Content is protected !!