Sanaa zilizoibwa miaka 130 iliyopita zarudishwa Afrika

HomeKitaifa

Sanaa zilizoibwa miaka 130 iliyopita zarudishwa Afrika

Mataifa mengi ya barani Ulaya na Marekani kwa miaka mingi yamekuwa yakishikilia sanaa mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika tangu enzi za ukoloni na hata nyuma ya hapo. Mataifa hayo yenye nguvu yamehifadhi rasilimali hizo kwenye makumbusho zao na wamekuwa wakipokea watalii wengi kutoka duniani kote.

Katika mchakato wa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na mataifa ya ulaya, mataifa ya Afrika kama Cameroon, Benin, Nigeria na Ethiopia, yamekuwa yakidai kurejeshwa kwa sanaa zao ambazo ni urithi na utamaduni wao. Mataifa ya Ulaya yameanza kuitika wito au ombi hilo la kurejesha sanaa hizo, ambapo siku ya Ijumaa 12 November 2021, Ufaransa imerejesha sanaa 26 kwa Taifa la Benin. Ufaransa ilikwapua kwa nguvu sanaa hizo miaka 130 iliyopita.

Sanaa hizo ziliibwa na Ufaransa mwaka 1892, ambapo kati ya sanaa hizo ni milango kutoka Ikulu ya Dahomey, kit cha mfalme pamoja na sanaa za ngoma za asili.

Sanaa hizo 26 kwa sasa zitahifadhiwa katika makumbusho ya Quidah kabla ya kusafirishwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Dahomey ambayo iko katika ujenzi hivi sasa. Dahomey ilikuwa ngome ya kifalme ambapo nyingi katika sanaa hizo, ziliibwa hapo.

Idadi ya sanaa 26 ni kubwa zaidi Ufaransa kuwahi kurudisha kwa moja ya yaliyokuwa makoloni yake, huku Benin ikiwa bado ina dai zai ya sanaa 5000 zilizoibwa na Ufaransa. Taifa la Ufaransa ukiacha Benin, bado lina linahodhi sanaa za mataifa mengine mengi ya barani Africa.

Takribani asilimia 90 ya sanaa kutoka barani Afrika zinaaminika kushikiliwa Ulaya. Makumbusho ya Quia Branty pekee inahodhi sanaa 70,000 kutoka barana Afrika. Ripoti ya 2018 iliyotolewa na Serikali ya Ufaransa inasema kati ya hizo 70,000, 46,000 zirudishwe barani Afrika, katika nchi zao.

Mataifa kama ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani nao wako chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Afrika kurejesha sanaa zao.

error: Content is protected !!