Sehemu 10 zinazoshikilia rekodi ya joto kali zaidi duniani

HomeUncategorized

Sehemu 10 zinazoshikilia rekodi ya joto kali zaidi duniani

Ni kweli hivi sasa Dar es Salaam jua linawaka sana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeshalitolea maelezo jambo hilo na kusema jua limesogea karibu zaidi dunia.

Hata hivyo Dar es Salaam sio sehemu yenye joto kali zaidi duniani. Kuna sehemu ambazo zimewahi kuwa na joto kali zaidi.

Zifuatazo ni sehemu kumi ambazo zimewahi kuwa na joto kali zaidi katika historia ya mwanadamu

1. Death Valley (Marekani)

Sehemu hiyo ambayo inapatikana katika jimbo la Calfornia, iliwahi kufikia nyuzijoto 56.7 (mwaka 1913) kiwango ambacho ni ngumu kwa mwanadamu kuweza kuishi.

Mwezi Agosti mwaka 2020, kiwango cha joto katika eneo hilo kilifikia nyuzijoto 54.4.

2. Ouargla (Algeria)

Hapo jua linawaka ni balaa. Ni kati ya sehemu za bara la Afrika iliyowahi kuwa na joto kali zaidi ambapo Julai 5,2018 joto la Ouargla lilifikia nyuzijoto 51.3.

3. Mitribah (Kuwait)

Julai 21,2016, Mitribah iliyopo Kaskazini mwa Kuwait iliripotiwa kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha joto kilichowahi kurekodiwa katika bara la Asia. Ilifikia nyuzijoto 53.9

4. Basra (Iraq)

Sehemu hiyo imewahi kufikia nyuzijoto 53.9.

5. Turbat (Pakistan)

Mwaka 2017 nyoto katika eneo hilo lilifikia nyuzijoto 53.7

6. Dallol (Ethiopia)

Eneo hilo lenye utajiri wa chumvi ilikuwa na nyuzijoto 41 kwa kipindi kuanzia mwaka 1960 hadi 1966.

7. Aziziyah (Libya)

Mji huo uliopo maili 25 kutoka mji mkuu wa Libya, Tripoli, ilikuwa inafahamika kama sehemu yenye joto kali zaidi ulimwengu hadi kufikia mwaka 1922 ilipofikia nyuzijoto 58.

Hata hivyo mwaka 2012 wataalam wa hali ya hewa walisema takwimu hizo hazikuwa za kuaminika.

Hata hivyo eneo hilo lina joto kalia mbapo mara nyingi linafikia nyuzijoto 48.

8. Quriyat (Oman)

Usiku wa Juni 26,2018, joto katika mji huo lilifikia nyuzijoto 42.6.

9. Dasht-e Loot (Iran)

Hili ni eneo la jangwa, watu hawawezi kuishi hapo. Ni kati ya sehemu za dunia ziliyowahi kuwa na joto kali zaidi ambapo kati ya mwaka 2003 hadi 2009 nyuzijoto katika eneo hilo zilifikia 70.7.

10. Bandar-e Mahshar (Iran)

Joto katika eneo hilo hufikia nyuzijoto 51.

error: Content is protected !!