Serikali yaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini

HomeKitaifa

Serikali yaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inaendelea kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Taifa.

Akizungumza Machi 01 ,2025 katika ziara yake mkoani Tanga, Mhe. Dkt. Samia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP) katika kufanikisha malengo ya maendeleo, huku akibainisha kuwa Serikali inaendelea kuvutia wawekezaji kwa kutumia sera wezeshi zinazozingatia mahitaji ya soko la ndani na la kimataifa.

“Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa, ndiyo maana tunaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia mitaji ya ndani na nje,” amesema Rais Dkt. Samia.

Amesema miongoni mwa mipango inayotekelezwa ni mradi wa ujenzi wa gesi ya LPG na GBP Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 50 katika Jiji la Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuongeza thamani ya rasilimali za nchi na kukuza uchumi wa bluu.

Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa LPG Terminal GBP Gas Mkoani Tanga tarehe 01 Machi, 2025.

Aidha, Rais Dkt. Samia alieleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma, ambapo ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu unatarajiwa kuimarisha biashara na kukuza uchumi wa mkoa wa Tanga.

“Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa wananchi wa Tanga na maeneo jirani, na Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kufungua fursa zaidi za kibiashara,” .

 

Pia Rais Dkt. Samia alikutana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ufanisi wa shughuli za bandari ili kuchochea biashara na uwekezaji.

“Bandari ya Tanga ni lango muhimu la biashara, hivyo Serikali imepanga kuboresha huduma zake kupitia miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 429,” amesema

error: Content is protected !!