Serikali yakaribisha wawekezaji mradi wa Dege Eco Village Kigamboni

HomeKitaifa

Serikali yakaribisha wawekezaji mradi wa Dege Eco Village Kigamboni

Serikali imetangaza kuwakabidhi wawekezaji mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kujiridhisha kuwa ni hasara kuendelea na ujenzi mradi huo.

Hayo yalibainishwa bungeni jijini Dodoma jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Weenye Ulemavu, Patrobas Katambi alipokuwa akijibu swali ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mariam Kisangi.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani kukamilisha majengo ya mradi wa Dege Beach-NSSF Mbweni kwa kuwa ni wa muda mrefu.

Akijibu swali hilo, Katambi alisema Serikali imefanya tathmini ya mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni na kujiridhisha kuwa itakuwa ni hasara kuendelea na ujenzi wa mradi huo.

Alisema kutokana na tathmini hiyo serikali imeamriwa mradi huo uuzwe kwa wawekezaji wengine.

“Kwa sasa Mfuko bado unaendelea na taratibu za kuwakaribisha wawekezaji wenye nia ya kutwaa eneo hili na kueleza nia ya kuununua mradi huo.

error: Content is protected !!