Serikali yapiga marufuku biashara 15 kwa wageni

HomeKitaifa

Serikali yapiga marufuku biashara 15 kwa wageni

Kwa mara nyingine tena, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ameonesha dhamira yake ya dhati ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake. Katika hatua mpya ya kulinda ajira na fursa za kiuchumi kwa Watanzania, Serikali imetangaza marufuku ya aina 15 za biashara kufanywa na raia wa kigeni.

Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu raia wa kigeni, hususan kutoka China, kufanya kazi ndogo ndogo ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania, kama vile uuzaji wa nguo katika maeneo ya Kariakoo, uwakala wa fedha na udalali wa nyumba.

Kupitia Amri ya Leseni za Biashara (Zuio la Shughuli za Kibiashara kwa wasio Raia), 2025, serikali imeweka zuio rasmi kwa wageni kushiriki kwenye sekta ndogo zifuatazo:

  1. Biashara ya bidhaa kwa jumla na rejareja (isipokuwa maduka makubwa ya rejareja – supermarkets)
  2. Huduma ya uwakala wa fedha kupitia simu
  3. Ufundi wa simu na bidhaa za kielektroniki
  4. Uchimbaji mdogo wa madini
  5. Uongozi wa watalii (tour guiding)
  6. Huduma za posta na usafirishaji wa vipeto
  7. Uanzishaji na uendeshaji wa vituo vya redio na televisheni
  8. Uendeshaji wa maeneo ya makumbusho
  9. Huduma za udalali
  10. Biashara ya forodha na usafirishaji
  11. Ununuzi wa mazao shambani
  12. Umiliki na uendeshaji wa mashine za kamari (isipokuwa ndani ya casino)
  13. Umiliki na uendeshaji wa viwanda vidogo
  14. Utoaji wa huduma za kusindika mazao madogo
  15. Biashara zingine ndogo ndogo zinazotajwa kwenye amri hiyo

Kwa mujibu wa serikali, lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi na uchumi wa taifa lao kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu kwenye sekta za kibiashara na huduma. Aidha, hatua hii inalenga kupunguza changamoto ya ajira, hususan kwa vijana.

GN NO. 487A OF 2025 -THE BUSINESS LICENSING (PROHIBITION OF BUSINESS ACTIVITIES FOR NON-CITIZENS) ORDER, 2025
error: Content is protected !!