Serikali yatoa ruksa kwa wahamiaji wa Msomera kuhamia vijiji vingine

HomeKitaifa

Serikali yatoa ruksa kwa wahamiaji wa Msomera kuhamia vijiji vingine

Serikali imeridhia maombi ya baadhi ya wananchi wanaohama kwa hiari yao kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika maeneo mengine tofauti na Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana, wakati akizungumza kwa njia ya mtandao kwenye mkutano wa kujenga uelewa kuhusu zoezi la uwekaji alama za mipaka katika pori Tengefu la Loliondo na Zoezi la uhamaji wa hiari la wakazi wa Ngorongoro.

“Serikali yetu sikivu chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kujali maslahi ya wananchi kutoa uhuru kwa wananchi waliamua kuhamia maeneo mengine kwa hiari yao,” amesema Waziri Chana.

Waziri Balozi Dk. Chana amesema ni ruhusa kwa wakazi hao kuchagua kwenda kuishi mahala wanapoona panafaa kwa kufuata taratibu zilizopo bila kuvunja sheria za nchi.

error: Content is protected !!