Serikali ya Tanzania imetoa tamko kwamba haina taarifa kuhusu shehena ya taka zenye sumu ya nuklia zilizokuwa zinasafirishwa kuletwa Tanzania.
“Hatujapokea taarifa yeyote kuhusu meli, lakini tutawasiliana na mamlaka husika kwa taarifa zaidi kuhusu meli hiyo”, amesema Katibu Mkuu Wizara ya Usafirishaji Bwana Gabrieli Magire.
Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba meli yenye shehena ya taka zenye sumu ya nuklia ilitia nanga katika Bandari ya Mombasa. Vyombo hivyo vya habari vimeripoti ya kwamba meli hiyo ilikuwa na dhamira ya kutekeleza taka hizo kwenye fukwe za Afrika mashariki ambapo zingehatarisha zaidi maisha ya watu.
Shehena hiyo ilibebwa kwenye meli ya MV Peraeus Voy, ambapo ilifichwa kwa siri ili ionekana kama mzigo wa makufuli au vipuli. Mzigo huo uligundulika baada ya Waziri wa Afya nchini Kenya kutoa tamko baada ya kupokea taarifa za siri kuwa, mzigo huo ulikuwa na sumu za nuklia.
Baada ya utafiti wa kina kufanyika, ilingulika kwamba mzigo huo ulitoka Mumbai India na ulikuwa ukielekezwa Tanzania. Wachunguzi walisema kuwa wana ushahidi ya kuwa mzigo huo ulidhamiriwa kuja kutupwa Afrika Mashariki, ya mzigo huu una sumu nyingi sana ambayo inaweza kuweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu.
Bado majadiliano yanaendelea katika bandari ya Mombasa kujadili hatua za kuchukua kuhusu mzigo huo ambao ulikuwa ukielekea Tanzania.