Sheria utoaji wa viungo vya ndani ya mwili mbioni kutungwa

HomeKitaifa

Sheria utoaji wa viungo vya ndani ya mwili mbioni kutungwa

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema serikali iko mbioni kuja na sheria itakayoruhusu wananchi kuchangia viungo vya ndani ya mwili ikiwemo figo.

Waziri Ummy aliyasema hayo juzi wakati akiweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Alisema hivi sasa kumekuwa na wimbi la ongezeko la magonjwa yasiyo ambukiza hususani kwa vijana na watoto yakiwa na gharama kubwa.

“Mfano ukifanya usafishaji wa figo ni kati sh 180,000 hadi 200,000 kwa siku na bahati mbaya madaktari wetu wakiona una Bima ya Afya wanaweza kukuambia hata mara tano kwa wiki au upate mtu akuchangie figo na Tanzania hatua sheria ya kuchangia viungo tunataka kuitunga.”

Aidha, Waziri Ummy ameziagiza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa waadiligu na kutenda haki katika sampuli zinazohusu ubakaji na vinasaba vya uhalali wa mtoto.

 

error: Content is protected !!