Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kocha wa makipa Muharami Said Mohammd ‘Shilton’ aliyekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) kwa tuhuma kukutwa na dawa aina ya Heroin hakuwa muajiriwa wa klabu hiyo.
Mapema leo DCEA imetangaza kukamata kwa watu 9 katika oparesheni akiwemo Muharami wakituhumiwa kukutwa na jumla la kilo 34.89 za Heroin.
“Simba ilimuomba na kukubaliana na Muharami kuwanoa makipa wetu kwa muda wa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta kocha wa magolikipa,” imesema taarifa ya Simba.
Taarifa ya menejimenti ya Simba imesema kwa mantiki hiyo klabu hiyo haihusiki na tuhuma zinazomkabili kocha huyo.