Taharuki yatanda watoto kuuawa na Fisi

HomeKitaifa

Taharuki yatanda watoto kuuawa na Fisi

Wakazi wa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga wamekumbwa na hofu kufuatia kuwepo kwa matukio ya watoto kuliwa na fisi. Katika matukio hayo watoto wawili mmoja mwenye umri wa miaka miwili na miezi kumi aitwaye Albert aliuawa ikiwa ni siku chache baada ya kufariki kwa mtoto Raphael Dotto mwenye miaka mitatu.

Diwani wa kata ya Kitangili, Mariamu Nyangaka amekiri uwepo kwa taharuki inayosababiswa na matukio hayo akisema ameitisha kikao maalumu kitakachohusisha makundi mbalimbali ya wadau watakaojadili jinsi ya kutatua changamoto hiyo.

> Mjue Bibi Titi Mohammed, Mwanamke aliyezishinda

Wazazi wametakiwa kuwa makini kuwalinda watoto hasa muda wa jioni kuanzia saa 12 ambapo kila mzazi anatakiwa ahakikishe mtoto wake yuko nyumbani, lakini pia wanatakiwa kuwa na namba za simu za viongozi pamoja na vitendea kazi kama vipenga, panga na vifaa vya kujihami.

Ofisa Idara ya Maliasili, misitu na Nyuki kutoka Halmashauri ya Manispaa hiyo, James Mduma alisema operesheni imeanza kufuatilia mfululizo wa matukio ya Fisi kuua na kujeruhi watoto chini ya miaka mitano katika maeneo mbalimbali na wanafanya hivyo kwa ukishirikisha maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Mwanza.

error: Content is protected !!