Taliban yatangaza kulitwaa bonde la Panjshir

HomeKimataifa

Taliban yatangaza kulitwaa bonde la Panjshir

Kundi la Taliban limesema kwamba limelitwaa bonde la Panjshir, ikiwa ni hatua za kuimarisha utawala wao nchini Afghanistan.

Eneo hilo linakaliwa na kundi la Panjshir ambalo haliungi mkono utawala wa Taliban nchini humo na hivi karibuni kumeripotiwa kuwepo mapigano baina ya pande hizo baada ya mzungumzo kuvunjika.

Panjshir ndilo eneo la mwisho nchini humo ambalo lilikuwa bado linaupinga utawala wa Taliban, hivyo kulitwaa eneo huo ni ishara kwamba huenda kundi hilo likaunda serikali karibuni.

Hata hivyo wapinzani hao wamekanusha taarifa za ushindi zilizotolewa na Taliban.

error: Content is protected !!