Tanasha ashindwa kulipa pesa ya upasuaji

HomeBurudani

Tanasha ashindwa kulipa pesa ya upasuaji

Mwanamuziki kutokea Kenya Tanasha Donna ambaye pia ni Mzazi mwenza wa muimbaji kutokea Tanzania maarufu kama Diamond Platnumz, kwa sasa Tanasha anazungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari nchini Kenya kutokana na kushindwa kulipa zaidi ya Shilingi milioni 17 anazodaiwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutengeneza umbo lake.

Tanasha aliingia mkataba na kampuni inayoitwa BBL ambayo inahusika na masuala ya kutengeneza maumbo kwa njia ya upasuaji ambayo alitakiwa afanyiwe upasuaji ili atakapopata umbile jipya atumie umaarufu wake na ushawishi alionao katika jamii kuitangaza kampuni hiyo lakini baada ya upasuaji Tanasha alishindwa kutimiza masharti ya mkataba huo na kutakiwa kulipa kiasi hiko cha pesa.

error: Content is protected !!