Tanzania kushiriki Mkutano wa Viongozi wa G20 kwa mara ya kwanza

HomeKimataifa

Tanzania kushiriki Mkutano wa Viongozi wa G20 kwa mara ya kwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atashiriki katika Mkutano wa Viongozi wa G20 utakaofanyika kwa mara ya kwanza kwa Tanzania. Mkutano huu utafanyika tarehe 18 na 19 Novemba 2024 huko Rio de Janeiro, Brazil, ukiwa na kaulimbiu ya “Kujenga Dunia Yenye Haki na Sayari Endelevu.”

Mwaliko wa kushiriki mkutano huu umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Brazil, Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva, na unatoa fursa kwa Tanzania kujadili na kushirikiana na mataifa mengine yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani katika masuala muhimu yanayolenga maendeleo endelevu na usawa wa kijamii.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huu ni hatua muhimu katika kuimarisha nafasi yake katika masuala ya kimataifa na kujenga mustakabali mzuri kwa wananchi na maendeleo endelevu ya taifa.

error: Content is protected !!