Mtandao wa U.S. News & World Report unaojihusisha na maswala ya safari na utalii umetaja maeneo 20 muhimu kwa watalii kutembelea Afrika 2025 ambapo Tanzania imeshika nafasi ya kwanza.
Maeneo bora ya kutembelea Afrika mwaka 2025 yanatokana na mchanganyiko wa utamaduni, gharama nafuu, na vivutio vya kipekee.
Tanzania imechukua nafasi ya kwanza, ikijulikana kwa safari zake, Mlima Kilimanjaro, na maajabu kama Ziwa Natron na Hifadhi ya Ngorongoro. Serengeti pia inatajwa katika nafasi ya Tatu kwa safari za wanyamapori wakati wa uhamaji mkubwa.
Nafasi ya pili imechukuliwa na Maporomoko ya Victoria, yanayovutia kwa ukubwa na mandhari yake ya kuvutia kati ya Zambia na Zimbabwe. Zanzibar, sehemu ya Tanzania, inatajwa kwa upekee wa fukwe zake tulivu, Mji Mkongwe, na vivutio vya kitamaduni.
Eneo la Nne ni Masai Mara nchini Kenya, likifuatiwa na Mauritius, Namibia, Cape Town, na Seychelles, ambayo inajulikana kwa uzuri wa fukwe zake. Rwanda inashikilia nafasi ya 14 kwa utalii wa Sokwe, huku Cairo na Luxor nchini Misri zikivutia kwa historia na urithi wa kale wa Misri.
Maeneo haya yanapendekezwa kwa watu wanaotafuta uzoefu wa kipekee wa bara la Afrika, kutoka safari za porini hadi historia na fukwe za kupumzika.
Orodha kamili ni:
1. Tanzania
2. Victoria Falls
3. Serengeti National Park
4. Masai Mara National Reserve
5. Mauritius
6. Namibia
7. Zanzibar
8. Cairo
9. Cape Town
10. Seychelles
11. Malawi
12. Madagascar
13. Nairobi
14. Rwanda
15. Luxor
16. Kruger National Park
17. Marrakech
18. Botswana
19. Ghana
20. Tunis