Tanzania yalisogelea Kombe la Dunia

HomeMichezo

Tanzania yalisogelea Kombe la Dunia

Katika mechi ilivyochezwa usiku wa jana kuwania kufuzu Kombe la Dunia katika dimba la Amaan huko Zanzibar kati ya Timu ya Taifa ya Wanawake U17 (Serengeti Girls) na Burundi, Burundi wameibuka na ushindi wa 1-2 dhidi ya wenyeji wao.

Wakiwa wameanza kuchoka huku wakikaribia kutamatisha dakika 90 za mchezo, dakika ya 83 inawaamsha tena wachezaji wa timu zote mbili baada ya mchezaji Bora Ineza kuifungia Burundi goli la pili, goli lililowapa ushindi timu hiyo.

Licha ya kupoteza mechi hiyo ya nyumbani, Serengeti Girls wataendelea na hatua nyingine ya kufuzu Kombe la Dunia kwani wana jumla ya mabao 5-2 dhidi ya Burundi.

Estella Gakima wa Burundi aliifungia timu yake bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kabla ya Rehema Mohamed wa Tanzania kusawazisha.

Katika mchezo wa ugenini nchini Burundi, Serengeti Girls waliichana nyavu ya wenyeji wao kwa goli 0-4.

Kufuatia matokeo hayo, Tanzania itaenda nafasi inayofuata kuchuana na Cameron au Zambia kati ya tarehe 19, 20 na 21 mwezi huu.

error: Content is protected !!