Tanzania yatoa wito wa amani kufuatia hali inayoendelea Mashariki ya Kati

HomeKimataifa

Tanzania yatoa wito wa amani kufuatia hali inayoendelea Mashariki ya Kati

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko matukio yanayoendelea kujitokeza katika eneo la Mashariki ya Kati. Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo na iko katika mawasiliano ya mara kwa mara na Balozi zilizopo katika eneo husika.
 
Raia wa Tanzania wanaoishi au wanaosafiri katika maeneo yaliyoathirika wanahimizwa kuwa makini, kuweka usalama wao mbele, na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka za nchi husika pamoja na Ofisi za Kibalozi za Tanzania.
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na jumuiya ya kimataifa katika kutoa wito wa kujizuia, kupunguza mvutano, na kutafuta suluhisho la amani kwa migogoro hiyo kwa kuzingatia misingi na kanuni zilizowekwa katika Hati ya Umoja wa Mataifa.
error: Content is protected !!