TCRA yatakiwa kuongeza uwezo wa kuchuja maudhui yasiyo na maadili

HomeKitaifa

TCRA yatakiwa kuongeza uwezo wa kuchuja maudhui yasiyo na maadili

Rais Samia Suluhu Hassan, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha inakuwa na vifaa na mifumo yenye uwezo wa kuchuja maudhui yanayosambazwa kupitia teknolojia na mitandao ya kijamii, ili kuzuia yale yasiyo na maadili kufikia wananchi.

Amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua. Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia na mitandao yana manufaa lakini pia yana madhara yanayohitaji kudhibitiwa.

Rais Samia amesema anapotaka kufahamu sababu za kuruhusiwa kwa maudhui yasiyo na maadili, amekuwa akielezwa kuwa changamoto inayokabili TCRA ni ukosefu wa vifaa vya kuyachuja, hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuchunguza mahitaji ya vifaa na mifumo ya kiteknolojia itakayosaidia kutambua na kuchuja maudhui yasiyofaa.

“Ukiwauliza TCRA kwa nini mnaachia hizi zisizo na maadili watakwambia hatuna vifaa, nendeni katizameni vifaa gani na ‘system’ gani vinatakiwa ili tuweze kuchuja yale yasiyo maadili tuache na yale yenye maadili yaingie kwa watu,” amesema Rais Samia.

 

error: Content is protected !!