Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 01 (Werner kurudi Bundersliga, Hatma ya Koeman Barcelona kuwekwa wazi Jumamosi hii)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 01 (Werner kurudi Bundersliga, Hatma ya Koeman Barcelona kuwekwa wazi Jumamosi hii)

West Ham huenda wakapata nafasi ya kumsajili Luca Pellegrini (22) huku mchezaji huyo wa Italia akijizatiti kupata nafasi ya kucheza Juventus (Calciomercato).

Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner (25) ataangalia tena mustakabali wake katika klabu ya Chelsea ikiwa atashindwa kurudi katika kikosi cha kwanza cha Thomas Tuchel, kukiwa na tetesi huenda akarejea Ujerumani mwisho wa msimu huu (Telegraph).

Paris St-Germain ilimtaka kiungo wa Liverpool na England Jordan Henderson, 31, kabla ya kufanikiwa kumsajili Lionel Messi (34) kwa uhamisho wa bure kutoka Barcelona msimu huu (Go podcast via GMS).

Chelsea bado inajadiliana na wakala wa Antonio Rudiger (28) kuhusu mkataba mpya (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah (22) anataka kuondoka Gunners, huku klabu za Leeds, Aston Villa na Brentford zote zikihitaji huduma za mchezaji huyo wa England (Ekrem Konur).

Kocha wa Liverpool Jugen Klopp anahitaji huduma ya winga wa Bayern Leverkusen Moussa Diaby (22) katika kikosi chake (Calciomercato – Italy)

Kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips (25) anakaribia kutia saini mkataba mpya na Leeds- kama anavyosema wakala wa mchezaji huyo pande zote “ziko tayari” kufanikisha mpango huo (John Percy via Telegraph).

Tamko la afisa mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke, la kupuuza ripoti kwamba mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 21, ana ‘makubaliano ya uhamisho’ na klabu hiyo, limemkasirisha wakala Mino Raiola (AS)

Real Madrid huenda wakafufua azma yao wa kumsaka mshambuliaji wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 34, dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari (El Nacional).

Barcelona wanamsaka kinda wa Sweden Williot Swedberg (17) Pia kiungo huyo ananyatiwa na klabu za Liverpool na AC Milan (Fichajes – Spanish).

Barcelona haitamfuta kazi kocha wake Ronald Koeman kabla ya kukipiga na mabingwa wa La Liga Atletico Madrid Jumamosi hii (Sport).

error: Content is protected !!