Njia 5 za kumaliza kabisa madeni yako

HomeUncategorized

Njia 5 za kumaliza kabisa madeni yako

Madeni yanaweza kukusababishia msongo wa mawazo na kukosa amani, hivyo ni muhimu kujua jinsi gani ya kupunguza madeni uliyonayo.

  1. Tengeneza pesa Zaidi
    Kama ulikua unatengeneza pesa kidogo jitahidi kuwa na vyanzo vingi vya kutengeneza pesa. Anzisha biashara na miradi mbalimbali au ongeza muda wako wa kufanyua kazi ili ikusaidie kupunguza madeni uliyo nayo. Unapopata pesa ya ziada cha kuzingatia ni kulipa madeni yako kwanza
  2. Zungumza na wanaokudai
    Kama deni lako linaongezeka riba kila baada ya muda na uwezo wako wa kulipa umepungua usikae kimya, zungumza na anaekudai umuombee kama inawezekana akupunguzie riba kwenye deni lako kwasababu riba inapoongezeka ndipo deni lako linazidi kuwa kubwa zaidi.
  3. Uza vitu ambavyo hauviitaji sana
    Deni linapokua limefikia kubwa au halivumiliki tena na hauna cha kufanya unaweza kuuza baadhi ya vitu vyenye thamani ulivyo navyo lakini kwa muda huo hauviitaji sana. Njia hii itakuwezesha kupata pesa ya kukusaidia kupunguza madeni uliyonayo.
  4. Usikope ili kulipa deni
    Kukopa pesa ili ulipe deni haitakusaidia kuondokana na madeni ila itakufanya uwe na deni jipya ambalo litaendelea kukuumiza siku baada ya siku, hivyo hautakiwi kukopa ili kulipa deni.
  5. Zingatia matumizi yako ya pesa
    Katika kipindi ambacho unatakiwa uwe makini zaidi na matumizi yako ya pesa ni wakati una madeni na unataka kuyamaliza, jibane kwenye matumizi yako ya kila siku ili upate pesa ya kupunguza deni.
error: Content is protected !!