Fahamu sifa za ndege ya Airbus A220-300

HomeKitaifa

Fahamu sifa za ndege ya Airbus A220-300

Kwa mujibu wa tovuti ya Airbus, Tanzania ndio nchi ya kwanza barani Afrika na ya tano duniani kumiliki ndege ya aina ya Airbus A220-300. Ukiachilia ndege mbili ambazo Tanzania inazipokea leo kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Karume visiwani Zanzibar, tayari Tanzania ilishapokea ndege yake ya kwanza Airbus A220-300 toka mwezi Disemba 2018.

Tovuti ya Airbus inaeleza kuwa ndege hii ndio toleo jipya kabisa katika matoleo ya Airbus. Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria kati ya 100-150, kiwango chake cha matumizi ya mafuta ni kizuri zaidi ukilinganisha na ndege nyingine na siti zake ni pana zinazomfanya mtu ajinafasi pindi anapoketi.

Ina urefu wa mita 38.7, ina kimo cha urefu wa mita 11.5 na urefu wa mbawa zake ni mita 35.1. Airbus A220-300 ina uwezo wa kusafiri kwa kasi ya Kilomita 840 kwa saa. Inatumia Injini ya “Pratt & Whitney PW1000G” ambazo sifa yake kubwa ni kutumia mafuta kidogo na pia ndege hizo zina teknolojia ya kupunguza sana kelele hasa wakati wa kutua ukilinganisha na matoleo mengina ya ndege za Airbus.

– Ndege hiyo ina uwezo wa kuruka angani umbali wa futi 41, 000 kutoka usawa wa bahari.

– Inahitaji uwanja wenye urefu wa mita 1890 kupaa vizuri, na urefu wa mita 1509 ili kutua vizuri.

– Inawezo wa kuruka ikiwa na uzito wa Kg. 69,853

– A220 -300 inauwezo wa kubeba mafuta lita 21,917. Kwa mara ya kwanza ndege hii imeruka tarehe 27 Februari 2015. #clickhabari

error: Content is protected !!