Anza Wikiendi yako na filamu hii ya ‘MIMI’

HomeBurudani

Anza Wikiendi yako na filamu hii ya ‘MIMI’

Katika filamu hii, mhusika (Mimi) anaigiza kama binti maskini mwenye ndoto za kuwa mwigizaji mkubwa lakini ndoto hizo zinakatishwa baada ya wanandoa wawili kufika kwenye kijiji chao wakiwa na shida ya kupata mtoto. Wanandoa hao walivutiwa na “Mimi” hivyo wakaahidi kumpatia kiasi kikubwa cha fedha iwapo atakubali kupandikizwa mbegu za mwanaume huyo mzungu ili awazalie mtoto.

Balaa linamkuta Mimi ambaye aliondoka kwa wazazi wake akiwadanganya anaenda kurekodi ‘movie’ na wazazi hao bila kujua wanamruhusu kuondoka, lakini baadae wanandoa hao wanaamua kuondoka kwenye kijiji hicho na kumuacha ‘Mimi’ akiwa mjamzito bila kumuaga.

Kujua ni nini kilitotea baada ya hapo ni vyema ukatumia wikiendi yako kuitazama filamu hii yenye visa vya kweli ambayo inaweza kuibua hisia ndani yako kutokana na maudhui yaliyomo.

error: Content is protected !!