Serikali kuongeza ndege nyingine 5

HomeKitaifa

Serikali kuongeza ndege nyingine 5

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali ipo katika mipango ya kununua ndege nyingine 5 ili kuliwezesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwa na ndege 16 ifikapo mwaka 2023.

Akizungumza katika mapokezi ya ndege 2 mpya aina ya Airbus 220-300 zilizopewa majina ya Tanzanite na Zanzibar katika uwanja wa Sheikh Abeid Karume, Zanzibar, Rais Mwinyi amesema kuwa mipango inaendelea ili kufikisha idadi hiyo ya ndege 16 ambapo mpaka sasa ndege ambazo tayari zimefika nchini ni 11.

Rais Mwinyi alisema sababu kuu zilizochochea Serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ni kujenga heshima na kulinda hadhi ya Taifa kwani likuwa aibu kwa Taifa kutokuwa na ndege hivyo mkakati wa Serikali ni kuongeza ndege 5 zaidi na kufikia ndege 16 ifikapo 2023.

Alisisitiza kwa kusema, kuimarisha na kuboresha huduma za usafiri wa anga, majini na nchi kavu, ni msingi muhimu wa uchumi wa Taifa na Mataifa yote duniani ili kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kuyafikia masoko ya Kimataifa kwa urahisi na pia kukuza sekta ya utalii. Amefafnua kuwa licha ya Tanzania kuwa ya pili kwa vivutio vingi vya utalii duniani, bado idadi ya watalii wanaoitembelea sio wengi kutokana na uwezo mdogo wa kusafirisha watalii kwa kuwa bado inategemea ndege za nje kuleta watalii.

error: Content is protected !!